Washirika wetu
Utambulisho kimataifa
Reliance ni kampuni yenye daraja ‘A’ kutoka Global Credit Rating (GCR), ikiwa na matawi yasiyopungua saba (7) nchini Tanzania kama ishara ya kujitolea kwetu katika kutoka huduma bora na kuwafikia watu wengi zaid na kuthibitisha uwezo wa kulipa madai kwa kiwango cha juu.





Wanahisa wetu
APA Insurance inajihusisha na bima za afya, vyombo vya majini, anga na hatari nyingine za bima kiujumla. Ofisi zake ziko Nairobi, Mombasa, Nakuru, Kisumu, na Nyeri, pia imeajiri zaidi ya wataalamu 130 waliofunzwa vizuri, na wenye uwezo wa kutoa huduma nzuri kwa wateja na kuhakikisha kampuni ina uhusiano wa muda mrefu na makampuni makubwa ya bima kupitia wataalamu wake, na ina uwezo wa kuhudumia wateja wakubwa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutoa huduma za bima.
APA Insurance imekuwa mshirika mkubwa wa bima kiujumla na kampuni Reliance Insurance Company Limited. Kufikia mwisho wa mwaka 2005, iliweza kupata mapato ya zaidi ya Bilioni Moja na Milioni tano (ksh) nchini Kenya.
Ilizaliwa kutokana na muungano wa biashara za jumla za Kampuni ya Bima ya Apollo Insurance Company Limited, na Kampuni ya Bima ya Pan Africa Insurance Company Limited, A P A Insurance Limited, ilianza na utajiri wa miaka tisini ya uzoefu uliochangiwa na mashirika ya malezi. A P A Insurance Limited ilisajiliwa mwaka 2003 na kuanza kazi zake tarehe 1 Januari 2004.
Kampuni ya Bima ya Pan Africa Insurance Company Limited, ilianzishwa mwaka 1946 huko Mombasa kama kama Indo – Africa Insurance Co Limited, Ilikuwa kampuni ya kwanza ya bima kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Nairobi mnamo 1964. Pan Africa Insurance ilisimamia bima za maisha na za jumla.
Apollo Insurance Company Limited ilikuwa kampuni ya kwanza ya bima iliyojumuishwa humu nchini, iliyoanzishwa mwaka wa 1977 huko Mombasa. Mnamo 1981 afisi ya Nairobi ilifunguliwa na mnamo 1997 ikawa Ofisi yake Kuu ikijulikana kwa ubunifu wake na uchangamfu, Apollo ilikua polepole na ujio wa kitengo cha Afya mnamo 1999, ikawa moja ya kampuni 10 bora za bima nchini Kenya, mnamo 2003 ikiandika malipo ya jumla ya zaidi ya KShs. Milioni mia nane na hamsini katika kitengo chake cha jumla.