Bima ya Safari
Unasafiri nje ya nchi?
Kumekua na hatari nyingi zinazohusiana na safari za kimataifa. Unaweza kusafiri kibiashara, kufurahi au kama mwanafunzi na ukuishia kukumbana na hali zisizotarajiwa. Hii inajumuisha gharama za matibabu ya dharura yanayotokana na ajali au ugonjwa wa ghafla, kupoteza mizigo, kupoteza pasipoti, kucheleweshwa kwa safari, n.k., Bila shaka ungependelea safari yako isiwe na usumbufu. Bima yetu ya Travel Guard hukupa ulinzi unaofaa kwa ajili ya aina yoyote ya dharura ambayo inaweza kukukabili safarini.
Kwa nini unaihitaji?
- Kimsingi kujilinda dhidi ya hasara za kifedha kutokana na hatari zinazohusiana na usafiri.
- Kwa ulinzi kamili kama msafiri wa nje ya nchi.
- Ni moja vigezo vya visa kwa baadhi ya nchi.
- Vyuo vikuu vingi vinahitaji bima hii kwa wanafunzi wanaosoma nje ya nchi.
- Makampuni ya Kimataifa ya waendeshaji watalii/wasafiri wanasisitiza juu ya kua nayo.
Pata Maelezo Zaidi Hapa!
Nani anaweza kunufaika?
- Mtu yeyote mwenye miaka hadi 70 (Zaidi ya 70 pia anaweza kufuzu).
- Raia yeyote wa Tanzania anayeishi Tanzania.
- Mkazi yeyote wa Tanzania anayeishi Tanzania.
Muongozo Sahihi
Pitia muongozo huu ili kufahamu zaidi. Unaweza kuchagua kipindi na huduma ili kukidhi mahitaji yako kwa bei nzuri.
Zingatia:
- Kiwango cha ulinzi wa matibabu unachohitaji.
- Thamani ya mali yako unayotaka ilindwe.
- Uvumilivu wako yanapotokea majanga.
- Muda wa safari yako.
Jedwali la Faida
Vifurushi hivi ni Pamoja na Bima ya Matibabu pekee, Kupoteza Mizigo Iliyopakiwa, Kucheleweshwa kwa Mizigo Iliyokaguliwa, Kupoteza Pasipoti, Dhima ya Kibinafsi, Kucheleweshwa kwa Kusafiri (wa anga Pekee), Utekaji nyara na Kughairi safari.
- Kurudi kwenye nchi yako.
- Sajili dai lako kwetu.
- Kusanya nyaraka muhimu zinazohitajika
- Unaweza pia kuwasiliana nasi ukiwa nje ya nchi iwapo kutatokea dharura yoyote.
Ni rahisi sana kuomba. Jaza tu fomu ya pendekezo na uturejee. Unaweza kupakua pendekezo hilo kutoka kwa Huduma kwa Wateja > Fomu za Pendekezo.
Tafadhali safiri kila wakati na cheti halisi cha bima. Hii pekee ndiyo itakupa haki ya kuwasilisha dai ukiwa nje ya nchi.
- Kiwango cha juu cha watoto wawili chini ya miaka 5 kwa kila familia wanalipiwa bure wanaposafiri na wazazi wote wawili.
- Mtoto yeyote wa ziada, 50% pekee ya malipo yanayotumika.
- Kiwango maalum cha familia ni mara 2.5 ya malipo ya juu zaidi (Kiwango cha juu cha watu wazima 2 + watoto 2 hadi miaka 18).
- Matatizo yanayotokana na ujauzito ndani ya miezi 6 ya kwanza yanashughulikiwa
Bima ya Ajali binafsi, kifo na ulemavu wa kudumu. Huduma za Matibabu ya Dharura na Uokoaji ikiwa ni pamoja na kurudishwa Tanzania na Huduma za Dharura za Meno.
- Bima ya mtoto mchanga na vile vile hadi miaka 70.
- Bima ya safari ya siku moja tu, isiyozidi mwaka mmoja.
- Bima inapatikana katika chaguzi mbalimbali.
- Malipo kulingana na umri na eneo.
- Nyongeza iliyoundwa maalum juu ya faida zinazopatikana.
- Ulinzi kamili popote duniani.
- Bima ya muda mrefu/safari nyingi inapatikana kwa mashirika na biashara.
- Wapigie simu tu na usubiri wakurudie.
- Pata idhini ya matibabu kuanza.
- Kupona na kurejesha afya.
Ili kutunza kile unachokithamini, hasa linapokuja suala la huduma za matibabu ya dharura, tumeweka hili katika mikono ya kitaalamu ili kuhakikisha unapokea huduma bora ya matibabu na usaidizi iwapo kuna madai yoyote.
Yafuatayo yanafanya hhduma hii kua maalum:
- Inapatikana kwa saa 24 kwa siku, siku zote 365.
- Inapatikana duniani kote.
- Kupiga namba zetu ni bure.
- Timu ya Washauri wa Matibabu na Madaktari waliobobea.
- Pata huduma ya matibabu ya haraka.
- Dhamana ya kulipa bili za hospitali.
- Pata vifaa vya dharura vya uokoaji hewa ikihitajika.
25,000 $

100,000 $

120 $

1,500 $

180 $

180 $

200,000 $

60 $

500 $

3000 $
